Jumanne 19 Mei 2026 - 23:30
Kiburi cha bandia cha Marekani na Wazayuni kimevunjwa mbele ya taifa la Iran

Hawza/ Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Sulaymaniyah Iraq amesema: Lengo la safari yangu lilikuwa kutoa shukrani kwa taifa la Iran na kupongeza ushindi mkubwa dhidi ya maadui; ushindi ambao ni fahari kwa Waislamu wote.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza mjini Sanandaj, Mamosta Sami Othman Faraj, katika safari yake kwenda Iran na kukutana na maulamaa pamoja na wanazuoni wa dini wa Mkoa wa Kurdistan, leo alisema katika hotuba yake: Lengo la safari yangu lilikuwa kutoa shukrani kwa taifa la Iran na kutoa pongezi kutokana na ushindi mkubwa dhidi ya maadui; ushindi ambao ni fahari kwa Waislamu wote.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Sulaymaniyah Iraq alisema: Kwa mujibu wa aya za Qur’ani, leo uadui wa Mayahudi dhidi ya Uislamu umejitokeza wazi zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Mamosta Othman Faraj alisisitiza kwa kusema: Wajibu wa wanazuoni wa dini ni kuwaelewesha, kuwafahamisha vijana kuhusu njama mbalimbali, na kueneza utamaduni wa kutetea ardhi pamoja na heshima ya nchi za Kiislamu.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Sulaymaniyah Iraq alisema: Baadhi ya nchi za Kiislamu zimegeuka kuwa vituo vya maadui, yaani Marekani na Israel, hali ya kuwa katika Uislamu imekatazwa kushirikiana na maadui wa dini.

Alibainisha kuwa: Hapo awali dunia ilikuwa ikiihofia nguvu ya Marekani, lakini kusimama imara kwa taifa la Iran na damu ya viongozi mashahidi kumeonyesha kwamba; kambi ya haki hupata ushindi kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha